Monday, September 6, 2010

LINI BAADHI YA MAGAZETI YA TANZANIA YATASEMA UKWELI?

LINI BAADHI YA MAGEZETI YA TANZANIA YATASEMA UKWELI?

BY VALENTIN

Katika gazeti la Mtanzania, la Agosti 25,2010 siku ya Jumatano lilitoa habari juu ya Msitu wa Loliondo 2. Kichwa cha habari Serikali yabariki msitu “Uteketetezwe”.

Katika habri hiyo tunaambiwa (umma/public) kuwa wananchi waanza kukata mkaa, lakini cha kushangaza hakuna hata taarifa ya ukataji wa miti na wananchi kwajili ya kuchoma mkaa na hata hiyo mada ya mkaa kama ilivyo tajwa kwenye kichwa cha habari cha gazeti haipo.

Kwa habari ambayo tunajua kuwa ikiwekwa kwenye gazeti basi umma wa Watanzania na wasiowatnzania ndani na nje ya nchi wanaweza kusoma na kuelewa kinachoendelea upande mwingine wa dunia. Ukisoma gazeti hilo ambalo limekuwa likiandika taarifa mbalimbali juu ya mambo yanayoendelea wilayani Ngorongoro utajiuliza swali rahisi kuwa Je ni wananchi gani wameshaanza kukata mkaa?halafu jamii inayokaa huko wanatumia jiko za aina gani?lakini ni mwezi tu umepita(25 Julai, 2010)Mkurugenzi wa Misitu Dr Kilahama alitangaza Msitu wa Loliondo 2 kuwa chini ya Kijiji na msitu huo umekuwa pale toka enzi za Ukoloni chini ya utunzji wa wenyeji wanaoishi pale hata kama hawajawahi kukabidhi rasmi na msitu ule umeendelea kutunzwa kwasababu weneyeji ni wahifadhi kwa asili yao.

Pia habari kwa kukoleza zaidi kuwa Uhai wa Loliondo sasa shakani. Ukisoma pia taarifa hiyo hakuna hata viashiria kuwa msitu huo sasa upo shakani ukizingatia kuwa hata kabla serikali kufanya mpango wa kuifanya Loliondo 2 kuwa msitu wa taifa tayari wananchi wanatunza bila hata kusuburi amri toka mamalaka yeyote.

Lakini cha kushangaza pia ni pale umma tunapoambia kuwa Mpango wa Serikali kukabidhi msitu huo kwa Wananchi umepokewa kwa pingamizi na hisia tofauti. Ila umma hatuambiwi kuwa ni pingamizi zipi na toka kwa nani au hisia zipi na zinatoka kwa nani zilizopokelewa.

Uwamuzi wa Msitu wa Loliondo 2 kuwa chini ya Kijiji umefikiwa na Kutangazwa na Mkurugenzi wa Misitu Dr Kilahama baada ya Filamu ya ‘Our Beloved Forest’ iliyotolewa na Maajabu Film chini ya Jumuiko la Maliasili Tanzania na kuoneshwa.

Wananchi katika Filamu hiyo wanaonyesha masikitiko yao jinsi walivyokuwa wanageuziwa kesi na halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro pale wanapowakamata wahalifu wanaokati miti ndani msitu. Uongozi wa halmashauri inawambia weneyeji kuwa hawana uwezo wa kuhoji uhalifu ndani ya msitu huo.

Uwamuzi wa Dr Kilahama ni sahihi ila taarifa zinazosambazwa ili kuangalia kama uwamuzi huo utatenguliwa si nzuri kwani wananchi wanozunguka misitu hiyo wanaujuzi zaidi wa namna ya kutunza Misitu ya asili kwani wamezaliwa na kukuwa katika mila na desturi zilizorafiki na misitu na wanathamini misitu kama wanavyo thamini maisha yao.

No comments:

Post a Comment